BORA KUZIMU YA BONGO

Jamaa mmoja alifariki na akapelekwa kuzimu, alipofika mapokezi akamkuta Shetani amekaa. Mazungumzo yao yakawa hivi:

Shetani: Ndugu yangu huku nafasi zilizobakia ni za kuzimu ya Marekani, Ufaransa na ya Tanzania pekee, sasa wewe unachagua uende kuzimu ipi?
Jamaa: Hebu nieleze kidogo juu ya kuzimu ya Marekani
Shetani: utakuwa unachapwa viboko 20 asubuhi na vingine 20 jioni kila siku kisha utakuwa unawekwa kwenye kiti cha umeme kuanzia saa sita hadi saa nane mchana kila siku.
Jamaa: Ya Ufaransa ratiba yao ikoje?
Shetani: Utawekwa kwenye kiti cha umeme kuanzia saa kumi na mbili mpaka saa mbili asubuhi kisha utachapwa viboko 20 na baadaye utachapwa vingine 20 jioni.
Jamaa: Mh! Basi nieleze ratiba ya kuzimu ya Tanzania kabla sijachagua
Shetani: Kutokana na tatizo la umeme kukatika mara wa mara siwezi kukutajia muda kamili utakaowekwa kwenye kiti cha umeme na pia Malaika wa kule ni mtumishi wa Umma hivyo huamua mwenyewe ni muda gani atakuwa ofisini na wakati mwingine huweza kuja kusaini tu na kuondoka bila kufanya kazi kwa hiyo sijui hizo fimbo zako arobaini utachapwa muda gani au unaweza usichapwe kabisa.

No comments: