Siku moja mwalimu alikuwa anasahihisha madaftari ya wanafunzi wake wa Chekechea, basi mara wakatokea Diana na Sosi ambao pia ni wanafunzi wake. Basi mazungumzo yakawa hivi:
Mwalimu: Enh watoto wazuri mnasemaje?
Diana (kwa udadisi wa kitoto): Eti mwalimu Mama yangu anawedha kupata mimba?
Mwalimu: Kwani mama yako ana miaka mingapi?
Diana: Arubaini
Mwalimu: Ndiyo anaweza kupata mimba
Diana (huku akitazama chini): Na mimi je nawedha kupata mimba?
Mwalimu (huku akitabasamu): Hapana Diana wewe bado mdogo sana huwezi kushika mimba
Sosi (ambaye alikuwa kimya muda wote akamshika Diana mkono): Mi thi nilikwambia muda wote ukawa unakataa thatha umethikia mwenyewe mwalimu naye amethemaje? Hatuna haja ya kuogopa.
1 comment:
kwi!kwi!kwiiiiiiiiiiiiii!!!!
Post a Comment